- Madaktari wa upasuaiji katika mji mkuu wa India Delhi wamefanikiwa kuwatenganisha wavulana pacha waliokuwa wameshikana katika kichwa.
- Wavulana hao wa miaka miwili Jaga na Kalia walifanyiwa upasuaji uliochukua takriban saa 16 na sasa wako katika chumba wagonjwa mahututi ICU, kulingana na madaktari.
- Kundi la madaktari 30 walifanya upasuaji huo katika taasisi ya matibabu na sayansi ya All India.
- Watoto hao walizaliwa wakiwa na wanatumia mishipa ya damu ya pamoja mbali na tishu za ubongo, hali isio ya kawaida ambayo hutokea mara moja kati ya watoto milioni 3 wanaozaliwa.
No comments:
Post a Comment